Raisi Samia, Aipongeza Yanga

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Caf kwa kuitoa Rivers United ya Nigeria 🇳🇬 kwa jumla ya mabao 2-0.

“Pongezi kwa Klabu ya Yanga kwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup), na kila la kheri katika maandalizi mliyoanza sasa kwa mchezo ujao. Mmeandika historia jalili. Mmetuheshimisha sana. Hamasa yangu inaendelea, na sasa imeongezeka. Kaifanyeni kazi,” Rais Samia.

Yanga itakutana na Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika nusu fainali huku mechi ya kwanza ikipigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa kabla ya marudiano Afrika Kusini.

Post a Comment

Previous Next

نموذج الاتصال